Umoja wa Ulaya yapanga kumfungulia vikwazo Mugabe

Umoja wa Ulaya katika mkutano wake wa mwaka utakaofanyika Februari unatarajia kujadili uwezekano wa kumfutia rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe zuio la kusafiri.

Mpaka sasa Umoja huo umeondoa vikwazo kadhaa vya kiuchumi ilivyowekewa Zimbabwe lakini ilibaki na msimamo mkali dhidi ya Mugabe na mkewe Grace.

Hatua dhidi ya Mugabe na familia yake zilichukuliwa miongo miwili iliyopita baada ya Jumuiya ya Kimataifa kuchukizwa na kile kilichoitwa ukiukwaji wa hali ya juu wa haki za binadamu na udanganyifu wa uchaguzi katika utawala wake.

Hata hivyo, mkongwe huyo alikanusha madai dhidi yake akisema badala yake Zimbabwe iliadhibiwa kutokana na sera yake ya umiliki wa ardhi.

Mugabe alilaumu vikwazo akisema vimechangia uchumi kuanguka. Wakosoaji wanasema hata hivyo kwamba uharibifu mkubwa umetokana na uwezo wake mdogo.

Mwakilishi wa EU nchini Zimbabwe Philippe van Damme hivi karibuni aliwaambia wanahabri kwamba vikwazo dhidi ya Mugabe vitapitiwa upya umoja huyo utakapojadili hali ya sasa ya Zimbabwe mwezi ujao.

"Kila mwaka kipindi kama hiki huwa naulizwa swali hilo hilo na mimi jibu langu linabaki lilelile. Ni uamuzi wa baraza litakalokutana Februari na mimi siwezi kusema watazungumzia nini," alisema van Damme.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia