Akizungumza na waandishi wa habari leo, mtoto wa mzee huyo aitwaye Maida Waziri amesema kuwa nyumba yao imetapeliwa na mpangaji wao aliyekuwa amepangishwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na baada ya mkataba wa malipo ulipoisha alitakiwa kulipia pango lingine lakini alikaidi akidai kuwa nyumba ni ya kwake na kwamba aliuziwa.
Amesema kuwa kabla ya mpangaji huyo kuuziwa nyumba na watu wasiojulikana, familia hiyo ilipata taarifa kwamba nyumba ilitaka kuuzwa na fedha zingepita benki ya Twiga Bancorp, hatua iliyowalazimu kupeleka zuio lakini benki hiyo haikufuata maelekezo hayo.
Maida amefafanua kwamba baba yake amekuwa mtumishi wa umma kwa takribani zaidi ya miaka 30 na alijenga nyumba zake wakati akiwa mtumishi wa serikali enzi hizo, pia nyumba hiyo hiyo anayodai kudhurumiwa amejenga kwa kipindi cha miaka 30 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka zaidi ya 90.