Jinsi ya kufanya ili kuepuka hatari ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa mMtu aliyebakwa

Moja kati ya maswali ambayo yalikuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali ni kuhusu je ni nini kinaweza kufanyika ili kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mtu alibakwa?
Kwanza kabisa unachotakiwa kutambua ni kwamba mtu aliyebakwa anatakiwa kuchukuliwa haraka ndani ya masaa 72 mara baada ya kufanyiwa kitendo hicho kisha kwenda kwenye kituo cha afya ili kupatiwa matibabu  ya haraka  iwezekanavyo.

Huduma hii hufanyika kwa mtu hii ni mara baada ya kugundua ameingiwa na majimaji yaliyotoka kwa muathirika wa virusi vya UKIMWI mwilini mwake au kwa kitalamu huitwa (PEP).

Baada ya hapo hufanyika vipimo hivyo vya haraka hii itapunguza uwezekano wa mtu huyo kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Na kwa jinsi huduma hii ya PEP Itavyotolewa haraka ndivyo mtu huyo aliyebakwa atakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kutopata maambukizo ya virusi vya ukimwi.

Hivyo Muungwana blog inakusiitiza elimu hii uliyoipata uwashirikishe na watu wengine ili tupunguze wimbi kubwa la waathrika wa ugonjwa huu wa UKIMWI.

Mpya zaidi Nzee zaidi