Magaidi 19 waangamizwa katika operesheni ya jeshi la Uturuki

Jeshi la Uturuki kataika operesheni yake dhidi ya ugaidi Afrin limewaangamiza magaidi 19 wa kundi la PKK/KCK/PYD-YPG  na kundi la wanamgambo wa Daesh.

Idadi ya wanamgambo ambao wamekwisha uawa katika operesheni hiyo ya jeshi la Uturuki imeongezeka na kufikia magaidi 1614 tangu kuanza kwa operesheni hiyo Januari 20.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na makao makuu ya  jeshi la Uturuki,  magaidi hao waliangamizwa katika opereshni ya anga ilioendeshwa na jeshi.

Jeshi la Uturuki kwa ushirikiana na jeshi huru la Syria  linaendelea kusonga mbele katika opereshni yake Afrin.
Mpya zaidi Nzee zaidi