Mashambulizi ya kujitoa muhanga yaua watu 21 Nigeria

Watu takriban 21 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakiwa wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kujitoa muhanga Nigeria.

Kwa mujibu wa habari,mashambulizi hayo yametokea katika soko moja la jimbo la Borno kaskazinimashairiki mwa Nigeria.

Wafuasi wa Boko Haram watatu ndio wanaoshukiwa kuhusika na shambulizi hilo.

Ripoti zinaonyesha kuwa watu 21 wamepoteza maisha katika mlipuko huo wakiwemo waliojilipua wenyewe.

Idadi ya waliopoteza masiha haikujulikana mpaka hapo Jumamosi asubuhi.
Mpya zaidi Nzee zaidi