Yanga hiyoo Robo fainali ya Shirikisho

Yanga imefanikiwa kusona mbele katika mashindano ya Kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Majimaji FC, mechi ikichezwa katika Uwanja wa Majimaji.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa pande zote mbili huku Majimaji wakiongoza kumiliki mpira, ulianza kutikiswa kwa nyavu za Majimaji kupitia Pius Buswita katika dakika ya 40.

Goli hilo la Buswita lilimaliza kipindi cha kwanza huku Yanga ikiwa mbele kwa matokeo ya 1-0.

Kipindi cha pili kilipoanza, dakika ya 52, Emmanuel Martin alifunga goli la pili kwa njia ya kichwa, akiunganisha krosi nzuri ya Hassan Kessy, na kufanya matokeo yawe mabao mawili kwa Yanga na sufuri kwa Majimaji.

Na katika dakika ya 61. Jaffar Mohammed, alifanikiwa kuipatia Majimaji FC bao la kusawazisha kwa njia ya kichwa na kufanya ubao wa matokeo kubadilika na kuwa 2-1.