Azam FC kumsafirisha mchezaji kwaajili ya matibabu


Mlinzi wa kati wa Klabu ya Azam FC, Daniel Amoah, anatarajia kusafirishwa kwenda jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya goti siku ya  Jumatatu ijayo Machi 26.

Amoah ameshindwa kupona majeraha hayo aliyoyapata Desemba 19, mwaka jana, wakati Azam FC ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Baada ya kupata matibabu Amoah alirejea dimbani Februari 7 kwenye mechi dhidi ya Simba ambapo Azam FC ikipoteza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, huku nyota huyo akijitonesha tena hali iliyomfanya kukaa nje ya dimba hadi sasa.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, ameweka wazi kuwa beki huyo ataenda kutibiwa katika Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo nchini humo na akiangaliwa kwa undani tatizo lake kwa muda wa siku nne.

Amoah anakuwa mchezaji wa tano wa timu hiyo msimu huu kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, wengine wakiwa ni Josepha Kimwaga, Mbaraka Yusuf, Shaaban Idd na nahodha Himid Mao ‘Ninja’ ambaye ametibiwa hivi karibuni na kupona kabisa.

Mpya zaidi Nzee zaidi