Hizi ndizo sababu za Mtu kukosa Usingizi Nyakati za Usiku

Tatizo la kukosa usingizi au kwa kitalamu, Insomnia ni tatizo endelevu linalosababisha mtu kushindwa kuanza kusinzia, kutodumu kwenye usingizi ama vyote viwili licha ya kupata fursa ya kulala ipasavyo. Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana. kukosa usingizi hakumalizi nguvu tu na hali yako, bali hudhuru afya na ubora wa maisha.

Usingizi kiasi gani unatosha hutegemea mtu moja na mwingine,mara nyingi watu wazima huhitaji masaa 7 hadi nane ya kulala.

Watu wengi pia walishawahi au watapata tatizo la kukosa usingizi kipindi fulani katika maisha yao lakini huwa si endelevu lakini baadhi wanaweza kupata tatizo hili na kuwa endelevu. Kukosa usingizi kupo kwa aina mbili yaani aina ya kwanza na aina ya pili amabayo husababishwa na madawa au ugonjwa mwilini.

Vifuatavyo ni visababishi vya kukosa usingizi.

Msongo wa mawazo
kuhusu shule, kazi, afya au familia huweza kusababisha akili yako ikafanya kazi usiku na kusababisha kushindwa kulala. Kipindi kigumu katika maisha kama kifo ugonjwa au kupoteza mpendwa, kuachika, kupoteza kazi huweza pelekea kukosa usingizi.

Wasiwasi
kupata wasiwasi kila siku husababisha tatizo la kukosa usingizi.

Msongo wa mawazo
Unaweza kulala kupita kiasi au kukosa usingizi kama una msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hutokea pamoja na matatizo mengine ya kiakili.
   
Hali ya kiafya
kama una maumivu sugu, upumuaji wa shida,au unakojoa mara kwa mara unaweza kupata tatizo la kukosa usingizi. Matatizo ya kiafya yanayoambatana na tatizo la kukosa usingizi ni maumivu ya michomo katika maungio, saratani, kufeli kwa moyo,ugonjwa kwenye mapafu,

Ugonjwa wa kucheua
GERD, kufanya kazi sana kwa tezi ya thyroid,kiharusi,ugonjwa wa parkinson’s na alzheimer’s.

Kubadili mazingira au ratiba za kazi
kusafiri au kufanya kazi joini au kuwa na shifti za kazi mapema huweza kubadili tabia ya mzunguko wa mwili na kusababisha kukosa usingiz. Tabia ya mwili huwa kama saa ya ndani ya mwili ambayo huongoza kila kitu kama mzunguko wa kulala na kuamkana michakato mbalimbali kwenye chembe hai mwilini na ujoto.

Kukosa ratiba ya kulala-
kukosa ratiba ya kulala kama kutokuwa na mda maalumu wa kulala, kazi za kuamsha mwili kabla ya kulala, mazingira yasiyo rafiki kwa ajili ya kulala, kutumia kitanda kwa kazi nyingine isipokuwa kulala ama kufanyia tendo la ndoa.

Madawa  
Madawa mbalimbali yanaweza kusababisha hali ya kukosa usingizi kama vile madawa ya kupambana na sononeko, madawa ya moyo na shinikizo la damu, madawa ya aleji, viamsha mwili kama Ritalin na corticosteroid. Madawa mengi ya dukani kama madawa ya maumivu, mabawa ya kuzibua pua na kupunguza uzito na matumizi.

Kahawa, nicotini na pombe
kahawa chai, cola na vinywaji vyenye virutubisho vya kahawa hujulikana kuwa ni viamsha mwili. Kunywa kahawa mchana au usiku huzuia mtu kupata usingizi usiku. Nicotine iliyo kwenye tumbaku na sigara huwa ni kiamsha mwili kingine kinachosababisha kukosa usingizi. Pombe hulegeza mwili na huweza kusababisha kusinzia lakini huzuia kufikia kilele cha usingizi na kwa kawaida husababisha kuamka wakati wa usiku.

Kula sana wakati wa jioni.
chakula kidogo ni sawa, lakini kula kupita kiasi wakati wa jioni au usiku huwea kukusababisha hisia za kutohisi vema kama ukilala chini na kusababisha kushindwa kusinzia.watu wengi pia hupata kiungulia, kubeua, ambavyo humkosesha usingizi.

Mpya zaidi Nzee zaidi