Na Paul Mabeja, DODOMA
Kamishana wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ROGERS WILIAM SIANGA amesema mamlaka hiyo imekamata lita laki 4 za kemikali bashirifu zilizokuwa zikiingizwa nchini na kutengeneza dawa za kulevya kwa njia za kienyeji.
Akizungumza mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya maswala ya ukimwi na dawa za kulevya mjini Dodoma SIANGA amesema pamoja na kukamatwa kwa kiasi hicho pia wamemkamata mtu mmoja ambaye alikuwa bingwa wa kuingiza kemikali hizo.
Amesema mtu huyo alijaribu kufanya kila njia ili kumhonga zaidi million 800 huku msaidizi wake akitakiwa kupewa million 400 kwa lengo la kushawishi apewedhamana.
Naye mtaalam wa dawa za kulevya PETER MFISI amesema kuna viashiria vya kuwepo kwa viwanda bubu vya kutengeneza dawa za kulevya nchini hivyo wananchi watolee taarifa pindi wanapoona kiwanda ambacho hakieleweki.
Akielezea changamoto wanazokutana nazo katika vita dhidi ya dawa za kulevya PETER MFISI amesema kuwa sheria ya dawa za kulevya zazubar imekuwa kikwazo katika vita hiyo kwani wauzaji wote wakekimbila huo wakijua hata wakikamatwa watapewa dhamana hivyo kuharibu kesi.