Milima na wingi wa mawe kisingizio cha kutopanda miti

Na James Timber, Mwanza
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza waishio milimani wamekuwa waoga katika suala la upandaji miti kwa kisingizio cha  kuwa miti haikuwi mahali palipo na mawe.

Akizungumza na Muungwana Blog kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Kikundi cha Mazingira katika eneo la Kliniki Kata ya Mirongo jijini Mwanza  Mzee Rashid Mwinyi, ameomba Serikali na Taasisi binafsi kuhamasisha wananchi kupanda  miti kwa maendeleo ya mji, ili wananchi wapate mwanga juu ya upandaji miti.

Mzee Mwinyi amesema rasmi walianza ujasiriamali wa kuhifadhi mazingira kwa kuotesha miti na maua toka mwaka 2014, ambapo walipewa eneo hilo na halmashauri, ambalo sio rasmi na kuiomba serikali kuwapa eneo la kudumu ili kuendeleza shughuli hizo.

Pia kikundi hicho kimekuwa kikitoa miti mashuleni kwa ajili kutunza mazingira katika shule za serikali kwani wanafunzi wengi wanapata shida uoteshaji miti, ambapo mara nyingi huishia kuharibika bado michanga.

"sisi tumekuwa tunatoa miti baadhi ya shule, japo hali ya sasa na hapo nyuma ni tofauti kwani awali wananchi waliitikia vyema sasa hivi mwitikio umepungua" alisema.

Kwa upande wake mmoja wa mjasiriamali aliyejiunga na kikundi hicho tangu kuanzishwa Bw. Mboka Manyema, ameomba vijana wasio na ajira waje kujiajiri katika kikundi kwani vijana wengi waliojiajiri katika kikundi hicho wamepata mafanikio makubwa.


Mpya zaidi Nzee zaidi