Rais Trump aonywa na viongozi wenzake kuingilia uchunguzi

Rais wa Marekani Donald Trump ameonywa na viongozi wenzake kutoka chama cha Republican kuhusu kuingilia kazi zinazofanywa na Robert Mueller anayeongoza jopo la uchunguzi ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Onyo hili limetolewa baada ya rais Trump kumshambulia Mueller kuhusu uchunguzi wake unaohusu tuhuma zav Urusi kuiingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Katika mtandao wake wa kijamii wa twitter rais Trump amesisitiza kuwa hakukuwa na ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi ambapo ameita uchunguzi wa Mueller kama wa kutafuta mchawi.

Aidha Rais Trump ameendelea kushutumu kuwa timu ya uchunguzi ya Mueller imesheheni watu kutoka chama cha Democrats.

Hata hivyo Mueller mwenyewe ambaye wakati fulani alisifika kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la FBI, ni mwanachama wa chama cha Republican.
Mpya zaidi Nzee zaidi