Korea kusini na korea kaskazini zimepanga tarehe ya kufanyika mkutano wa kilele, kufuatia mkutano wa ngazi ya juu ambao ulifanyika baada ya kiongozi wa Korea kaskazini yenye silaha za kinyuklia Kim Jong Un kufanya ziara yake ya kwanza kimataifa nchini China.
Kwa mujibu wa nia ya viongozi wote wa Korea kaskazini na kusini wamekubali kufanya mkutano wao Aprili 27 katika nyumba ya amani mjini Panmunjom, imesema taarifa ya pamoja, iliyosomwa na viongozi wa ujumbe wa pande hizo mbili.
Mkutano huo kati ya Kim Jong Un wa Korea kaskazini na rais Moon Jae-In utakuwa wa tatu wa aina hiyo, na utafuatiwa na mazungumzo ya kihistoria na rais wa Marekani Donald Trump mapema mwezi Mei mwaka huu.
Hatua hiyo imeonekana kumpa moyo Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anapambana kutaka kutisishwa matumizi ya silaya za nyuklia baada ya uongozi wa China na Korea Kaskazini kukutana.