https://monetag.com/?ref_id=TTIb Trump kuiongezea ushuru wa forodha China | Muungwana BLOG

Trump kuiongezea ushuru wa forodha China

Rais Donald Trump ametangaza mpango wa ongezeko la ushuru wa forodha kwa bidhaa za China,hali hiyo inatarajiwa kuongeza vita vya vikali vya kibiashara ambavyo huenda vikawa na madhara kwa mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani.

Hata hivyo ametia saini hati ya maelekezo kwa maofisa juu ya namna ya kushughulikia suala la ushuru kwa bidhaa za mabilion ya dola zinazoingizwa kutoka nchini China.

Trump amesema awali aliiona China kama rafiki,lakini amebaini kuwa vikwazo vinahitajika baada ya kugundua kuwa China inaonekana kutaka kujinufaisha kijanja katika uendeshaji biashara ambao umekuwa ukiingizia Marekani hasara ya mabilion ya dola kila mwaka.

Amesisitiza kuwa China ni moja kati ya mataifa anayokusudia kuingia katika majadiliano ya kibiashara.

"Ndiyo tumeanza majadiliano na umoja wa ulaya,kwa sababu wametuwekea vikwazo,kuna mazingira ambayo yanawaruhusu kufanya biashara na sisi,lakini sisi hatuwezi kufanya biashara na wao.Wana vikwazo vikubwa dhidi yetu,wana ushuru wa forodha mkubwa sisi hatuna,siyo haki.Nao NAFTA wamekuwa wabaya kwetu,lakini tutajitahidi kurekebishana ama kufanya kitu cha ziada. Mpango wa kibiashara na Korea Kusini ni wa upande mmoja,unatakiwa kufanyiwa mabadiliko.Kwa hiyo kuna mambo mengi yanayotokea,lakini kwa suala la Uchina tutatumia kifungu 301 ambacho kitahusisha dola billion 60 ambazo ni sehemu tu ya hiki tunachokizungumza''Trump

Hatua hii ya rais Trump dhidi ya China imekuja,kufuatia uchunguzi wa mwezi August kuhusiana suala la forodha ambao uliagizwa kufanyika na Trump mwenyewe.

China kwa upande imeonya na kuongeza kuwa iko tayari kujibu mashambulizi ya kibiashara dhidi ya Marekani na imeituhumu Marekani kwa kukiuka sheria za kimataifa za kibiashara.