Idadi yapungua ya wahamiaji waliozuiliwa

Idadi ya wahamiaji wanaozuiliwa nchini Libya imepungua kwa kiasi kikubwa tangu kutolewa kwa taarifa ya biashaa ya utumwa.

Kiongozi wa idara ya serikali iliyoundwa kwa ajili ya kukabiliana na biashara haramu ya uhamiaji Jenerali Mohammad Bishr, amesema idadi ya wahamiaji waliozuiliwa na serikali ilipungua kutoka 27,000 mwezi Mei hadi 5,200.

Amesema hali hiyo iliwezesha kufungwa vituo 20 vya kuwazuilia wahamiaji nchini humo kati ya vituo 53 tangu mwezi Mei 2017.

Inaelezwa kwamba kupungua kwa idadi hiyo kulitokana na mchakato wa kuharakisha kuwarejesha nyumbani wahamiaji, hasa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji – IOM huku pa mataifa kadhaa ya kiafrika yakiwarejesha nyumbani mamia ya raia wao, hasa tangu ripoti ya shirika la habari la CNN iliyoonyesha kuwepo kwa soko la watumwa nchini Libya.
Mpya zaidi Nzee zaidi