Rais Macron ataka viongozi wake kuueshimu muungano wa demokrasia huria

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewataka viongozi wa Ulaya kuulinda muundo wao wa demokrasia huria katika wakati huu ambapo kuna tawala za kimabavu kote ulimwenguni na demokrasia zisizo na huru ndani ya Umoja wa Ulaya.

Macron amewaambia wabunge wa Umoja wa Ulaya mjini Strasbourg kuwa mabadiliko makubwa yanayoshuhudiwa ulimwenguni yanawahitaji wanasiasa kubadilisha mbinu zao, lakini hilo halimaanishi kuikataa demokrasia.

Aidha amelalamikia tabia ya kuulaumu Umoja wa Ulaya kila wakati serikali zinapokabiliwa na mapungufu, na kuepuka kuzungumzia mustakabali wa Umoja wa Ulaya.

Hotuba ya Macron katika bunge la Ulaya imekuja wakati Umoja wa Ulaya unajiandaa kwa uchaguzi wa bunge mwezi Mei 2019, ikiwa ni wa kwanza wa aina hiyo tangu Uingereza ilipoamua kujiondoa katika umoja huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi