Mufti Mkuu wa Tanzania aitaka Bakwata ibadilike

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, amesema, wakati umefika kwa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania, BAKWATA kubadilika ili kuweza kuendesha shughuli zake kiuweledi na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea ikiwa lengo ni kuwaunganisha Waislaam.

Mufti Zuberi ametoa rai hiyo Mjini Dodoma leo wakati akifunga mkutano mkuu wa siku mbili wa Bakwata ambapo amesisitiza haja ya baraza hilo kuelekeza nguvu zake katika kuwahudumia waumini wa dini ya Kiislaam nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Sheikh Ali Abdallah Ali , amesema, mkutano huo umewasilisha mapndekezo ya maazimio 32 kwa lengo la kulijenga baraza hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi