Wapinzani wa Yanga kuwasili Jumatano au Alhamisi

Klabu ya soka ya Yanga inajiandaa kuwapokea wapinzani wao wa Kombe la Shirikisho Walayta Dicha ambao wanatarajiwa kuwasili nchini kati ya Jumatano na Alhamisi wiki hii kutokea nchini Ethiopia kwaajili ya mchezo wa mtoano.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kurejea leo jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Singida ambako jana jioni kilicheza mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Africa na kutolewa na Singida United.

Walayta Dicha inashika nafasi ya nane kwenye Ligi ya Ethiopia inayoshirikisha timu 16 wakiwa na jumla ya pointi 23. Hata hivyo bado hawajatoa taarifa rasmi ya idadi ya watu watakaokuwa katika msafara huo.

Yanga na Walayta Dicha zitacheza mchezo wa kwanza April 7 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo nchini Ethiopia. Mshindi wa jumla ataingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mwaka juzi Yanga pia ilishiriki michuano hii baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Al Ahly ambapo ilicheza na Esperanca ya Angola kwenye kombe la Shirikisho na kufuzu hatua ya makundi.

Mpya zaidi Nzee zaidi