Urusi yawekewa vikwazo vipya

Muakilishi wa Marekani Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema kuwa Marekani itaiwekea vikwazo vipya Urusi na mashirika mengine ambayo yanahusika na  mpango wa sialaha za kemikali nchini Syria.  Hayo Nikki aliyazungumza Jumapili na kusema kuwa vikwazo mihvyo huenda vikachukuliwa Jumatatu.

Katika mahojiano aliofanya katika runinga ya CBS News, Nikki  amesema pia kuwa malengo ya Marekani Syria haijawahi kuwa kumuondoa madarakani Assad bali kuzuia  vita na kutuma ujumbe. Ujumbe ambao haukufafanualiwa.

Akizungumza kuhusu Marekani na Syria  uwezekano wa maazungunzo, Haley amesema kuwa serikali ya Assad haina umuhimu  kushirikishwa  katika  mazungumzo Washington.