Waganga wa jadi huchangia ongezeko la vifo na migogoro katika jamii

Wananchi wa Kijiji cha Bukuba  Wilaya ya Buhigwa katika  Mkoa  Kigoma wameonywa vikali kwenda  kwa waganga wa jadi kupata matibabu kwani huchangia ongezeko la vifo katika jamii hasa kwa Mama na watoto.

Akizungumza na Wandishi wa Habari katika Uzinduzi wa Zahanati ya Ilakoze kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mratibu wa Damu Salama wilayani humo Bw. Notas Makuna amewataka wananchi kutotumia waganga wa kienyeji kutibu matatizo yao badala yake watumie vituo vya afya na zahanati zilizopo kumaliza matatizo hayo.

Joshua  Kabega ni Mkazi wa Kijiji hicho alisema walikua wanatembea  umbali mrefu kutafuta huduma ya  afya, na kutumia   gharama za matibabu pamoja na ukosefu wa madawa kwa wakati, zitapungua baada ya kuanzishwa kwa Zahanati mpya ndani ya kijiji hicho.

“Tunashukuru sana kwa kujengwa kwa zahanati hii tutafaidika sana hasa katika kijiji chetu cha Bukuba, Kibuye na Nyakoronko kwa miaka mingi tumekua tukihangaika  kutembea kwa mwendo mrefu na hata tukienda bado tunarudi bila kupata dawa katika hospitali hizo," alisema Mkazi huyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bukuba Bw. Wiston Kayanda ambaye ni Mkurugenzi wa Zahanati hiyo, alisema  imeanzishwa zahanati  kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi kiafya kuwepo changamoto mbalimbali kama vile  vifo vinavyotokana na kukosekana kwa huduma muhimu na  haraka.

Kayanda alisema migogoro mingi katika familia na jamii ni waganga wa jadi wasio na vibari maana  wanafanya biashara wengi wao wamekuwa wachonganishi na waongo, ambapo amewataka wananchi na vijiji vilivyoko jirani watumie zahanati hiyo kwa ajili ya matibabu na huduma za huakika.