Wanawake Lindi na Kilwa wafunguka sababu za wanaume kukataa na kutelekeza watoto

Na.Ahmad Mmow
IMEELEZWA kwamba miongoni mwa sabababu zinazochangia wanaume kuwakataa na kuwatelekeza watoto ni baadhi ya wanawake kukosa uaminifu na kuchagua wanaume wakuwapa watoto kwa kigezo cha uwezo wa kiuchumi.

Hayo yamebainishwa leo nabaadhi ya wanawake  wa waliotoka katika wilaya za Lindi na Kilwa mkoa wa Lindi, katika vijiji vya Pande ploti,Mikoma,Dimba na Kilolambwani.Ambao walishiriki warsha ya kupambana na ukatili Wa kijinsia,iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Wakizungumza kwenye warsha hiyo kupitia mradi wa miaka minne wa kupinga ukatili wa kijinsia unaofadhiliwa na shirika la misaada la kimataifa la OXFAM-Tanzania,nakutekekezwa na shirika la kiraia la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto Lindi (LIWOPAC).Walisema wanawake wasio waaminifu kwenye ndoa na wanaochagua wanaume wakuwapa watoto na mimba kwa kigezo cha uwezo wa kiuchumi wanachangia sababu za watoto kukataliwa na kutelekezwa na wanaume.

Sofia Mwandazi wa kijiji cha Nakimwela Mikoma alisema wanaume wanapobaini kuwa mtoto wanaye mlea hatokani na damu yake anakuwa hana upendo na mtoto huyo hata kama amezaliwa ndani ya ndoa.Hali ambayo inasababisha ndoa kuvunjika na mtoto kutelekezwa.

Alisema nijambo lakusikitisha kuona mila potofu zinachangia wanawake wakose uaminifu katika ndoa zao nakusababisha  ndoa nyingi kuvunjika na kuchangia watoto kukataliwa na waume zao.

" Nyakanga anakufundisha kwamba ukijenga nyumba kubwa lazima ujenge na kibanda ili nyumba kubwa ikijaa ukalale kwenye kibanda.Au ukiwa na ndoo uwe na kidumu mkononi kwasababu maji ya kwenye ndoo yakimwagika ubaki na maji ya kwenye kidumu.Yote hayo nikutuhimiza tuwe na wanaume nje ya ndoa ili wawe kama akiba,"alisema Sofia.

Mwanamke huyo alisema kwabahati mbaya sana mara nyingi watoto wa nje ya ndoa wanafanana sana na baba zao wazazi. Kwahiyo wanaume wanapogundua hawawezi kuwakubali watoto hao.Bali huwakataa na kuwapa talaka wake zao.Huku wakishindwa kuwampa wanaume waliozaa nao.Kwa hofu yakujulikana walizini.Hivyo kujikuta wakitunza na kumlea watoto peke yao na kuanza kulaumu waliokuwa wauwe zao kwamba wamemtelekezewa watoto.

Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Biana Moris wa kijiji cha Kilolambwani alisema baadhi ya wanawake sio wakweli na  wanawabambikia mimba na watoto wanaume wenye uwezo wa kiuchumi na kuwanyima wanaume waliowapa mimba kwakuwa ni maskini.Ambapo wanaume wote wawili wanapogundua kwamba mwanamke huyo ni muongo wanaamua kumkataa mtoto au mimba.

Alibainisha kwamba baadhi ya wanawake wasioolewa wanapokuwa na mimba wanakuwa na kadi za kliniki zaidi ya moja zenye majina ya wanaume tofauti ya waliowapa mimba hiyo.Huku wakiendelea kupata huduma kutoka kwa wanaume wote.Hata hivyo wanaume hao wakibaini kwamba mimba hiyo inawahusu wanaume wengi huikataa.

"Muda mwingine nisisi wanawake wenyewe tunachangia watoto kukataliwa na wanaume.Lakini tunalalamika sana,kwabahati mbaya sana wanaume wengi hawapendi kueleza ukweli wanaogopa fedheha na kujidhalilisha.Lakini pia kukosekana uvumilivu ndani ya ndoa no chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika"matokeo yake watoto wanatelekezwa.Baadhi ya wanaume wanawapenda watoto wakiwa pamoja na mama zao tu," alisema mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Hadija Nambea.

Maelezo ya wanawake hao ambayo yalitokana na mada iliyouliza sababu za watoto kutelekezwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili,yaliungwa mkono na Farijala Mchopa wa Kilolambwani aliyesema japokuwa wanaume wamekuwa wahanga wa kutelekezwa watoto lakini baadhi ya akina mama wanamchango mkubwa katika kukataliwana kutekezwa watoto.Huku akiongeza kusema maelezo na malalamiko ya wanawake dhidi ya wanaume yanapewa uzito hata kama yauongo.Wakati wanaume hata wakisema kweli wanaonekana waongo.

Warsha hiyo iliwashirikisha pia viongozi wa dini,wazee na maofisa watendaji kata wa kata za Kilolambwani na Pande.Ambapo mwishoni mwa warsha hiyo ilipendekezwa vijijji vilivyopo kwenye utekelezaji wa mradi huo unaotekelzwa kwa awamu ya mwaka mmojammoja, vitengeneze sheria ndogo ambazo zitataka wanandoa kushirikiana matumizi ya mapato ya familia,kuuza na kununua pamoja mali za familia,kupanga uzazi kwa pamoja,kushirikiana katika kuoa na kuozesha na kuwashirikisha watoto katika kufanya maamuzi yanayohusu familia.

Kwa upande wake maratibu wa mradi huo ambae pia alikuwa mwezeshaji wa warsha hiyo,Michael Mwanga alitoa wito  kwa jamii kufuatilia kwakaribu vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa  kwa mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wanaotenda vitendo hivyo
Mpya zaidi Nzee zaidi