Taarifa zinaeleza kuwa klabu ya Yanga ina matumaini makubwa kuwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa kiungo wake, Aziz Ki, itafutwa baada ya klabu hiyo kuwasilisha rufaa kupinga adhabu hiyo.
Licha ya Yanga kutotoa taarifa rasmi, inadaiwa inaendelea na hatua za kisheria kwa lengo la kuhakikisha Aziz Ki anapatikana kwa ajili ya mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba, unaotarajiwa kuchezwa baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Klabu hiyo inaamini kuwa rufaa yake itazingatiwa na kadi hiyo kuondolewa, jambo litakalomuwezesha Aziz Ki kushiriki katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
