Bado hatujaamua nchi gani itakua mwenyeji ufunguzi AFCON 2027


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Septemba 17, 2026, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amebainisha kuwa, mwenyeji wa mechi ya ufunguzi wa michuano ya AFCON 2027, bado hajajulikana.

Kulingana na Motsepe, uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji wa mechi hiyo, unatarajiwa kufikiwa hivi karibuni.

Michuano ya AFCON 2027, inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda kuanzia Juni 19, 2027 hadi Julai 17, 2027.

Kwa kuzingatia matayarisho ya nchi husika, hususani miundombinu ya viwanja, unadhani mechi ya ufunguzi inastahili kuandaliwa na nchi gani?

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi