China yafungua mkutano unaohudhuriwa na Urusi, Irani Marekani yajitoa


China leo (09.06.2018) imefungua mkutano wa siku mbili wa usalama wa kanda unaohudhuriwa na Urusi, Iran na washirika wengine, kutokana na Marekani kujitoa katika makubaliano ya kinyuklia na Iran.

Magari  ya  deraya  yamejipanga  mitaani  katika  mji  wa  pwani  wa Qingdao wakati  viongozi wa  dunia  wakiwasili  siku  ya  Ijumaa  kwa ajili  ya  mkutano  huo  wa  18  wa  kila  mwaka  wa  shirika la ushirikiano  la  Shanghai (SCO), kundi  la  kimkoa  la  usalama linaloongozwa  na  China  na  Urusi. Mataifa  wanachama  ni  pamoja na  Jamhuri  nne  za  iliyokuwa  Umoja  wa  Kisovieti  katikati  ya bara  la  Asia , Pakistan  na  India. Iran  ni  mwanachama mwangalizi.

Maafisa wamewaondoa  watu wote  katika  eneo  la  ufukwe  la  mji huo, wakiwaondoa  watu  wanaofanya manunuzi , wakaazi  na  watu wanaotembelea  eneo  hilo kuwezesha  rais  wa  China Xi Jinping , mwenzake  wa  Urusi Vladimir  Putin  na  rais  wa  Iran Hassan Rouhani kupita.

Rais  wa Pakistan Mamnoon Hussain  na  waziri  mkuu  wa  India Narendra Modi  pia  watahudhuria  mkutano  huo.

Mkutano  huo  wa  SCO unakuja  baada  ya  rais  wa  Marekani Donald Trump  kuiondoa  nchi  hiyo  katika  njia  ya  utata  kutoka katika  mkataba  wa  kimataifa  wa  mwaka  2015 na  Iran  ambao unaweka  ukomo  wa  mpango  wake  wa  kinyuklia  ili  kuweza kulegezwa vikwazo  vya  kiuchumi.

Licha  ya  kwamba  suala  hilo  halimo  katika  agenda  rasmi , wachambuzi  wanasema  kwamba  mada  muhimu  ya  majadiliano mwaka  huu  huenda  ikalenga  juu  ya  iwapo Iran itaruhusiwa kutoka  katika  nafasi  yake  kama  mwangalizi  wa  mkutano  huo  wa SCO  na  kuwa  mwanachama  kamili, hatua  ya  maendeleo ambayo  inaiwania  tangu mwaka 2008  lakini  imeshindwa kufanikisha  kwa sababu  ya  vikwazo  vya Umoja  wa  Mataifa.

Makubaliano  ya  kinyuklia  ya  mwaka  2015  yameondoa  kizingiti hicho.

Hivi  sasa kutokana  na  kujiondoa  Marekani  kutoka  katika mkataba  huo, "Wanachama  wa SCO huenda  wakatumia  fursa hiyo  kuipa Iran  uanachama kama  njia  ya  kuonesha  kuiunga mkono pamoja  na  makubaliano  hayo  ya  kinyuklia," amesema dawn Murphy , profesa wa  mitaala  ya  usalama  wa  kimataifa katika  chuo cha  Marekani  cha  vita vya  angani.

Wasiwasi  kuhusiana  na  Iran unakuja  wakati  suala  lingine la kinyuklia  linajitokeza , ambapo  Trump  na  kiongozi  wa  Korea kaskazini  Kim Jong Un wanajitayarisha  kwa  ajili  ya  mkutano mjini Singapore.

Masuala  ya  biashara, uwekezaji  na  ushirikiano  wa  maendeleo pia  yatakuwa  mada  muhimu  katika  mkutano  huo  wa  SCO, Murphy  amesema , kutokana  na hali  ya  hewa  ya "ongezeko la kupambana  na  utandawazi  na mbinyo  katika  taasisi  za  dunia  za uchumi  wa  mataifa", unaoongezwa makali  na  sera  za  Trump  za kizalendo  za "Marekani  kwanza".

Mataifa  ya  SCO huenda  yakajadili  uwezekano wa  eneo  huru  la kibiashara  la  pamoja, alisema , wakati  China  pia  inajaribu kusukuma  ushiriki  katika  mradi  wake  wa  miundo  mbinu ya ukanda  na  barabara  ya  dunia.

"Mataifa  wanachama  wa  SCO wanataka  mafanikio ya  juhudi  za ukanda  huo  na  barabara pamoja  na  kuongezeka  kwa  ushawishi wa  China ikiwa  kama  nguvu  kuu