Mfahamu muigizaji Van Damme Kiundani zaidi

Van damme ni mwigizaji, muongozaji, mtenengezaji, mwandishi wa filamu, mpiganaji wa kickbox, taekwondo, karate, alishapigana mapambano kadhaa ya kweli na kushinda. van damme alianza kufahamika rasmi mwaka 1976.

Jina lake halisi  anaitwa  (jean claude camille francois van varenberg) alizaliwa tarehe 18/10/1960 mji wa brasells nchini ubeligiji. Kwa sasa  jean claude camille francois van varenberg   ana umri wa miaka (56). Pia majina yake mengine ya  utani anafahamika kama jvcd, van damme, the musles from brassells.

Wazazi wa van damme baba ni waloon anazungumza kifaransa, mama flemish anazungumza kiholanzi.

Maisha yake ya ndoa.
van damme ameshaoa wanawake wanne katika maisha yake ambao ni maria rodriguez 1980-84,cyncthia derderian 1985-86,gladdys portuguse 1987 na kumuoa rasmi 1999.

Amefanikiwa kupata watoto watatu 3 ambao ni biancabree, kristopher, na nicholas,

Baadhi ya filamu alizofanya na kumfanya kujulikana ni pamoja na;


  • Bloodsport 1988
  • Lionheart,1990
  • Double impact 1991
  • Universal soldier 1992
  • Hard target 1993
  • Street fighter na time cop 1994
  • Sudden death 1995
  • Jvcd 2008
  •  Expandable 2 2012 na zingenezo nyingi.


Van damme ameshinda tuzo kadhaa za ubora wa filamu zake na kumpatia utajiri wa dola milion 30 taslim.
Mpya zaidi Nzee zaidi