Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema serikali haitazivumilia shule zitakazoshindwa kuwahakikishia wanafunzi usalama wao wawapo masomoni huku akionya udhalilishaji unavyofanywa na baadhi ya walimu kwa wanafunzi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
Waziri Prof. Ndalichako anatoa kauli hiyo wakati akikabidhi zawadi kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kuhitimu darasa la saba kidato cha nne na sita ambapo amesema udhalilishaji wowote dhidi ya mwanafunzi ni kinyume na sheria na serikali haiko tayari muvumilia vitendo hivyo.
Kuhusu sakata la udhalilishaji lililoripotiwa kufanywa na mwalimu wa shule ya msingi St Florence dhidi ya wanafunzi wake Waziri Prof Ndalichako amesema vyombo vya dola vinalifanya uchunguzi kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa kwa mwalimu huyo.
Katika hafla hiyo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amepongeza hatua ya serikali ya kukarabati shule kongwe kwani itarudisha ushindani wa kielimu ambao ulisaidia taifa kupata wanafunzi bora ambao walileta mchango mkubwa katika maendeleo
Kwa upande wake mwakilishi kutoka serikali ya Uingereza ambayo imekuwa mstari wa mbele kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Bi getrude Mapunda amesema nchi hiyo itaendelea kusaidiana na Tanzania katika sekta ya elimu.
