Huenda tukashuhudia usiku wa leo Gerard Pique akiandika historia yake mpya kwenye ligi kuu ya Hispania.
Mchezaji huyo endapo atacheza kwenye mchezo wa leo ambao Barca watakuwa ugenini dhidi ya Real Valladolid, huo utakuwa mchezo wa 300 kwa beki huyo kisiki.
Tayari Pique ameshacheza michezo 299 kwenye ligi hiyo ambapo Barca ameichezea michezo 277 na Zaragoza michezo 22 kipoindi ambacho alitolewa kwa mkopo na Manchester United kwenye msimu wa 2006 mpaka 2007.
Akiwa katika La Liga mchezaji huyo amefunga magoli 25 huku akiziongoza timu zake kupata ushindi kwenye michezo 220, sare 54, kufungwa michezo 25. Pia kwenye ligi hiyo ameshuhudia akipewa kadi za njano 79 na nyekundu 7.
