Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameibuka upya baada ya kusemwa vibaya sana kutokana na video iliyosambaa mitandaoni akionekana akiwa na Diamond Alhamisi hii kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Romy Jons iliyofanyika Samaki Samaki, Masaki.
Video hiyo imeonekana kuibua maneno mengi huku watu wakimcharua madam Sepenga kuwa bado wanamahusiano na Diamond huku wengine wakienda mbali zaidi wakidai anajipendekeza kwa ex wake huyo.
Wema ameshindwa kuvumilia maneno hayo na kuamua kujibu mapigo kupitia mtandao wa Instagram ili ujumbe uweze kuwafikia wabaya wake hao. Kupitia mtandao huo Sepetu ameandika.
After all being said... Let me take this opportunity to say something very Short & Clear...
.
.
.
I DONT LIVE MY LIFE ACCORDING TO WHAT PEOPLE WANT ME TO DO...I LIVE MY LIFE ACCORDING TO WHAT I WANT TO DO...
.
.
.
Mambo mengi mmesema only after video za Snapchat... Really...??? Kama ni matusi nimezoea mnooo ila tu nimeona bora niulize... Kwani nikisnap na Naseeb mbona kunakuwa na mgongano & nikisnap na watu wengine inakuwaga poa tu...??? Gimme a Break please... Watu tusifanye kitu kisa kuogopa watu... Tumekua sasa maisha mengine lazima yaendelee... MSIKARIRI MAISHA... Ni kosa kubwa sana... .
.
.
🖤Happy Saturday loves🖤
