Jengo la benki kuu lawaka moto


Moto umeripotiwa kuwaka katika benki kuu mjini Moscow.

Kulingana na vyombo vya habari vya Urusi, moto huo ulianza katika ghorofa ya tano ya jengo hilo.

Wazima moto wamefanikiwa kuuzima moto bila mtu yoyote kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Uchunguzi zaidi wa chanzo cha moto huo unafanyika.
Mpya zaidi Nzee zaidi