Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, ametangaza kuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan atazikwa Alhamisi ya Septemba 13, 2018 nchini humo kwa heshima kubwa.
Rais Akufgo ametoa tangazo hilo Akufo-Addo baada ya kukutana na familia ya marehemu Annan katika mji mkuu wa Accra.
Kofi Annan alikuwa mmoja wa watu wenye upeo mkubwa wa kizazi hiki. Alikuwa kama ndugu. Litakuwa tukio kubwa kwa nchi yetu ... Natarajia viongozi wengi watahudhuria," imesema taarifa hiyo ya rais Akufo-Addo.
Annan alifariki dunia Agosti 18 mwaka huu nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aliiwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1997 hadi 2006.
