Shirikisho la soka duniani FIFA, limemfungia miezi 12 kutojihusisha na soka rais wa shirikisho la soka nchini Palestina, Jibril Rajoub.
FIFA imemfungia rais huyo kutokana na madai ya kuwashawishi mashabiki wa soka nchini Palestina kuchoma jezi na picha za mchezaji Lionel Messi mapema mwaka huu ili kupinga timu ya taifa ya Argentina kucheza na Israel.
Pia Jibril atatakiwa kulipa faini ya kiasi cha dola 20,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 45v za Kitanzania.
Soma maelezo ya barua hiyo hapa chini:
The 12-month match suspension imposed on Mr Rajoub entails a ban on taking part in any future match or competition taking place during the given period," said FIFA in a statement.
Consequently, Mr Rajoub will not be able to attend football matches or competitions in any official capacity, which includes, among others, participating in media activities at stadiums or in their vicinity on matchdays.
He was also fined $20,000 by FIFA.
