Mbowe amfariji Rais Magufuli baada ya kufiwa na dada yake

 Wengi wetu tunafahamu kwamba Rais Magufuli amefiwa na dada yake aitwae Monica Joseph Magufuli ambaye amefariki asubuhi ya 19 Agosti, 2018 katika Hospitali ya Bugando Mwanza akiwa na miaka 63 huku akiacha Watoto 9 na Wajukuu 25.

Watu mbalimbali maarufu wa Tanzania wametuma rambirambi zao kwa Rais Magufuli akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambae alitumia ukurasa wake wa Instagram akiweka picha nyeusi isiyo na kitu na kuandika yafuatayo  “Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na wana CHADEMA wote, natoa pole na salaam za rambirambi kwa Mh.Rais @MagufuliJPM kwa kufiwa na dada yake Monica Magufuli, Mungu awape faraja, na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi”

Mpya zaidi Nzee zaidi