Mkuu Shule aliopigwa mwanafunzi na mwalimu hadi kufa asimamishwa


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Mratibu wa Elimu wa kata ya Kibeta, Hashim Upunda, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibeta Enetha Isdory na Msaidizi wake Sundi Elisha  kusimamishwa kazi pamoja na kuivunja kamati ya shule hiyo kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya walimu  jambo ambalo limekuwa kichocheo mauaji ya kikatili yaliyomkuta mwanafunzi wa darasa la tano Spelius Eradius.

Mauaji hayo yalifanywa na mwalimu Respicius Patric aliyedaiwa kumpiga mwanafunzi huyo hadi mauti yalipomkuta baada ya kumtuhumu kuiba mkoba wa mwalimu Elieth Gerald.

Brigedia Jenerali Gaguti ametoa agizo hilo alipofika shuleni hapo baada ya kukutana na walimu na wanafunzi katika shule, akizungumza amesema walimu hao watakuwa nje ya kazi ili wapishe uchunguzi wa kamati aliyoagiza iundwe na uongozi wa Manispaa ya Bukoba kwa lengo la kuchunguza vitendo  vinavyodaiwa kukithiri katika shule vya walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi bila kufuata taratibu.
Mpya zaidi Nzee zaidi