Lukuvi atoa onyo kali kwa wapimaji ardhi, atishia kuwafuta


Waziri wa ardhi William Lukuvi amesema serikali itazifuta kampuni za upimaji ardhi zinazoenda kinyume na taratibu ikiwemo wapimaji ardhi wasio waaminifu.

Lukuvi ameyasema hayo kupitia  hotuba yake  iliyosomwa na kaimu mkurugenzi  idara ya upimaji  na ramani  Dkt. James Mtakamaya wakati akifungua mkutano wa mwaka  wa  taasisi ya wapima ardhi nchini IST.

Naye Rais wa taasisi hiyo Mpima Martins Chodota amesema wameiomba serikali kupunguza  kodi ya vifaa vyao vya upimaji kwani vitu vya bei ya juu na vikiingizwa nchini vinalipiwa kodi kubwa.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo akiwemo Mpima Daudi Msungu amesema sheria zinazoongoza upimaji  zimepitwa na wakati na hivyo umefika wakati zifanyiwe marekebisho ili kuweza kuendana na hali halisi.
Mpya zaidi Nzee zaidi