Ujerumani kuandaa Euro 2024, Uturuki yalilia kutoswa


Ujerumani ndio itakayokuwa mwenyeji wa mashindano ya Euro 2024 baada ya kuipiku Uturuki katika kinyang'anyiro cha farasi wawili cha kutafuta kibali. Uamuzi huo wa UEFA umeisikitisha Uturuki.

Mabingwa hao wa Dunia mwaka 2014 walipigiwa kura hiyo na wanachama 17 wa kamati kuu ya UEFA. Uamuzi huo wa UEFA ni wa kusikitisha kwa upande wa Uturuki ambayo pia ilishindwa katika ombi lake la kuandaa michuano hiyo katika mwaka wa 2008, 2012 na 2016.

Waziri wa Vijana na Michezo wa Uturuki Mehmet Kasapoglu amesema kuwa uamuzi wa kuipa Ujerumani haki za kuandaa Euro 2024 ni wa kuhuzunisha kwa UEFA.

Amesema ni wazi kwamba Uturuki ilikuwa imejiandaa vyema kabisa kwa ajili ya dimba hilo kwa sababu ina vifaa na viwanja vipya.

Ujerumani iliandaa Kombe la Dunia 2006, lakini haijawahi kuandaa Euro kama nchi iliyoungana. Maana Iliyokuwa Ujerumani Magharibi iliandaa tamasha hilo mwaka wa 1988.
Mpya zaidi Nzee zaidi