Na. Thabit Madai,Zanzibar.
Msichana aliejulikana kwa jina moja Asma mkazi wa Mwera anatafutwa na Jeshi la polisi Mkoa wa mjini magharib kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya Mama aliejulikana kwa jina la Zubeda Yahya abdallah hadi sasa chanzo cha kuchoma moto nyumba hiyo bado hakijajulikana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa mjini magharb Unguja Thobias Gesauda Sedoyeka alisema jeshi la polisi mkoa wa mjini linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo aliekimbia kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya bi zubeda yahya abdallah miaka 22 mshirazi wa mwera.
Alisema moto huo umesababisha hasara ya kuunguza vitu vingi vilivyomo ndani ya nyumba hiyo ambapo hasara yote iliyotokea inakisiwa jumla shilingi million mbili na laki tano za kitanzania.
