Na.Thabit Madai,Zanzibar.
Jeshi la polisi mkoa wa mjini magharib limefanikiwa kuwakamata jumla ya Vijana watano kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi katika maeneo tofauti tofauti ndani ya mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Thobias Gesauda sedoyeka Alisema jeshi la polisi mkoa wa mjini linaendelea na operesheni zake mbali mbali na kufanikiwa kuwakamata jumla ya Vijana watano kwa kukutikana na dawa za kulevya aina ya bangi katika kipindi cha wiki moja.
Alisema vijana hao waliokamatw ni Idrisa Mamsuka Idrisa Miaka 27 Mzaramo wa mweza ambapo alikamatwa akiwa na furushi moja la bangi, kassim haji khamisi miaka 48 mgunya na mkazi wa masingini ambapo alikamatwa na nyongo 134 za bangi na Seif Ali Salum miaka 18 mshirazi wa mchanagani amekamatwa akiwa na nyongo 7saba za bangi.
Aidha kamanda sedoyekea aliwataja wengine ni Said chum mohameed miaka 27 mkaazi wa bububu alikutwa na nyongo 16 za bangi pamoja Huseein Ali miaka 20 mkazi wa Magomeni alikamatwa na nyongo 18 za bangi.
Hata hivyo kamanda alieleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kwa kipindi cha wiki moja na wote bado wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuchukuliwa hatua mbalimbali za kisheria.
