Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Ferooz amesema kuwa kwa wasanii kuna pokuwa na matabaka kuna kuwa na bifu na mwisho wa siku wanashindwa kusaidiana.
Ferooz amesema kuwa "Kitu chochote lazima mkae pamoja kuna pokuwa na vikundi kuna kuwa na matabaka matabaka kuna kuwa na bifu mwisho wa siku mnashindwa hata kusaidiana mwisho wa siku unakuta matatizo mengi mwisho wa siku hata msanii akipata matatizo msanii anashindwa kuface msanii mwenzie amsaidie anaona aibu anaoona ni bora amcheki pedeshee au bosi nani."
Ameongeza "Nilishakuwa na marafiki wengi, kwahiyo unapokuwa kwenye pick fulani unakuwa na marafiki na nilikuwa na mzunguko wa watu wengi ikafikia hatua nashindwa kujua yupi rafiki wa kweli yupi muongo kwahiyo nikawa nawaamini marafiki zangu kupitiliza ndio maisha jinsi yalivyo."
