Marioo: Namtamani sana Vanessa Mdee nifanye naye


Msanii wa Muziki, Marioo amesema kuwa anamtamani sana msanii wa kike Tanzania, Vanessa Mdee (Vee Money) kufanya nae.

Marioo amesema kuwa anamshukuru, Vanessa kwa kumpa fursa ya kufanya nae ngoma hivyo anatamani na yeye siku moja mashirikishe.

"Kwanza namshukuru sana Madam, Vee money kwa kunipa fursa ya kufanya nae ngoma moja na yeye nafikiri wakati ukifika itatoka, Lakini mimi pia na mtamani kwenye kazi yangu nifanye nae lakini nafikiri ngoma yangu nyingine itakayo toka kabla ya hii nadhani mwakani ntaanza kutoa ngoma tofauti tofauti nilizoshirikishwa watu wake tayari kujua Marioo ameshirikisha nani, wasanii tofauti tofauti," amesema Marioo.

Marioo kwasasa anatamba na kibao cha ngoma yake mpya inayoitwa 'Ifunanya'.
Mpya zaidi Nzee zaidi