![]() |
| Mkuu wa Chuo cha CBE, Emmanuel Mjema |
Na James Timber, Mwanza
Chuo cha Biashara (CBE), kinahitaji kadirio la kiasi cha shilingi bilioni mbili kutoka kwa wadau na wahitimu wa chuo hicho kwa lengo la kuboresha huduma ya mafunzo itolewayo na mendeleo mbalimbali ikiwemo miundombinu rafiki kwa baadhi ya wanafunzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa (CBE) Kampasi ya Mwanza, Mkuu wa Chuo Emmanuel Mjema amesema kuwa chuo hicho kilikuwa miongoni mwa vyuo vya kwanza kutoa elimu ya biashara hapa nchini, jambo lililopelekea kila mhitimu kupata ajira ya kudumu katika taasisi mbalimbali ikiwemo serikali.
"Nina waomba wahitimu CBE tukutane kwa pamoja ili tuzungumze masuala mbalimbali kuhusu chuo chetu pia tunakaribisha maoni yao na kuyafanyia kazi inapowezekana, pia na sisi tutaeleza changamoto zetu ili tusjadili kwa pamoja ni namna gani tunaweza kutatua nina imani tutafanikisha vyema, kama baadhi ya vyuo vinavyoendelea hua vina desturi ya kukutana na wahitimu kwa ajili ya mchango wa maendeleo, amesema Profesa Mjema.
Aidha amesema kuwa chuo kina maeneo mbalimbali kwa ambayo yapo kwa ajili ya kupanua wigo wa chuo ambapo wamefungua kampasi eneo la Kangae katika Kata ya Mecco Wilaya ya Ilemela kwa lengo la kuwapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kwa weledi.
"Sisi tumejihakikishia kutoa elimu iliyo bora inayomjengea mwanafunzi kupata kazi au kufikia malengo pale ahitimishapo elimu yake katika chuo chetu na mifano iliyo hai tunayo, hapa kuna waliomaliza chuo hiki wamepata ajira katika taasisi mbalimbali binafsi na serikalini huku wengine wakipiga hatua kubwa kiuchumi, amesema Mjema.
