Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, Swedi Mkwabi, amefunguka na kusema kuwa hakuna simba bora bila yanga bora na kukiri kuwa kwasasa yanga wanatetereka kutokana na masuala ya uongozi wa klabu.
Mkwabi ameyasema hayo katika hafla ya kupongezwa kwake kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba SC iliyo andaliwa na tawi la Simba Veteran Mango Gadeni ambapo alikuwa mgeni rasmi.
