Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, amewapiga dongo watani zao wa jadi Simba.
Ten ambaye alikuwa pia Kaitaba, ameandika machache kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuwakejeli Simba kuwa wamekuwa wakishinda mechi za ugenini pekee.
Ofisa huyo ameandika dongo hilo ikiwa watani zao Simba watoke kutoa sare tasa na Lipuli FC katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa wiki jana.
Aidha, Ten ameandika hivyo kutokana na mashabiki wengi wa Simba kuibeza Yanga kuwa itaendelea kushinda mechi za nyumbani Dar es Salaam pekee na ikishaanza ugenini ;nje ya Dar es Salaam' mambo yatakuwa tofauti.
Maajabu yameonekana katika mechi zote mbili ambazo Yanga imecheza nje ya jiji la Dar es Salaam, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC huko Shinyanga na Kaitaba hapo jana dhidi ya Kagera Sugar.
