Jinsi ya kupunguza au kuondoa maumivu ya kichwa wakati wa ujauzito.
byMuungwana Blog 1-
0
Wanawake wengi hupata tatizo la kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito.
Hili tatizo huweza kutokea wakati wowote wa ujauzito lakini mara nyingi
hutokea wakati wa trimester ya kwanza (miezi mitatu ya kwanza) na
trimester ya tatu (miezi mitatu ya mwisho) ya ujauzito.
Katika miezi mitatu ya kwanza kuumwa kwa kichwa mara nyingi
husabababishwa na kuongezeka kwa hormone na damu inayosukumwa mwilini.
Kuumwa kwa kichwa kunaweza kuongezeka zaidi pale mwanamke mjamzito akiwa
na stress, kukosekana kwa usingizi, uchovu, mafua, kuwa na low blood
sugar(sukari isiyotosha kwenye damu), ukosekanaji wa maji ya kutosha
mwilini(dehydration), kwa wale waliozoea kunywa kahawa kuacha kunywa
kahawa kunaweza kusababisha kuumwa kwa kichwa.
Kuumwa kwa kichwa wakati wa trimester ya mwisho husababishwa na
kuongezeka kwa uzito unaoweka stress kwenye mwili, mwili kutokuwa
balanced, pamoja na wanawake wengine kuwa na high blood pressure wakati
wa ujauzito(preeclampsia).
Mara nyingi mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa zozote zile kwa kipindi
hiki kwasababu kuna uwezekano wa dawa kupokelewa na mtoto na kumdhuru
kwa namna moja au nyingine. Hii ni sababu maalaamu kujaribu kutumia njia
natural kupunguza maumivu yoyote yale mama anayopatwa nayo kwa kipindi
hiki.
Jinsi ya kupunguza au kuondoa maumivu ya kichwa wakati wa ujauzito
Jaribu kutuliza misuli ya uso na kupumzika.
Uwe makini na madawa ya aspirin na jamii za dawa hii, kwa vile dawa yoyote uinywao inaweza kumuaffect mtoto.
Ukisikia maumivu jaribu kunywa maji glass 2 - 3, kwasababu wakati
mwingine maumivu husababishwa na kukosa maji ya kutosha mwilini.
Fanya zoezi la kutembea halafu kunywa maji mengi ya kutosha.
Pumzika vya kutosha na kupata mazoezi ya relaxation.
Fanya mazoezi mara kwa mara kama unavyotakiwa kwa mama mjamzito.
Kula chakula chenye afya kwa mama mjamzito.
Unaweza kuweka kitambaa cha moto kwenye eneo la macho, pua na kichwa
kama kuuma kwa kichwa kunasababishwa na mafua au weka kitambaa cha
baridi kwenye sehemu inayouma kama ni maumivu ya kichwa ya kawaida.
Hakikisha unabalance kiasi cha sukari kwenye damu(blood sugar)yako
kwa kula kiasi kidogo cha chakula kila baada ya muda mfupi badala ya
kusubiri kwa muda mrefu halafu kula mlo mkubwa.
Ukipata massage ya shingo, mabega na uti wa mgongo itapunguza stress na kupunguza maumivu ya kichwa.
Pumzika kwenye chumba chenye giza halafu jaribu kuvuta pumzi na kuachia ili kuondoa stress mwilini.
Oga maji ya moto au baridi.
Baadhi ya vyakula vinaweza kuchangia kuumwa kwa kichwa. Unaweza kujaribu
kuvitoa kwenye diet yako kuona kama vitasababisha kupunguza maumivu ya
kichwa.
Hivi vyakula ni pamoja na:
Chocolate
Vinywaji vikali
Mtindi, jibini, sour cream
Karanga
Mikate yenye yeast
Nyama zilizowekwa kemikali ili kuzisaidia kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.(processed milk)
Ongea na daktari kama umejaribu vitu hivi na bado maumivu yapo au
yanazidi au kuumwa kwa kichwa kunaambatana na kizungu zungu, kuvimba kwa
mwili, maumivu kwenye maeneo ya juu ya tumbo au kuongezeka kwa uzito
ghafla.