Kocha wa Simba: Timu nyingi za kiarabu nazitambua hasa kutokana na uzoefu nilionao


Patrick Aussems ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba SC, amefunguka kuwa anatambua ugumu wa mchezo wake wa kesho dhidi ya waarabu kutoka Algeria, JS Saoura ila ana imani na kikosi chake kitafanya vizuri kupata matokeo kwa kuwa anajua mbinu za wapinzani wake.

Kesho Simba watacheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wakiwa kundi D na JS Saoura ya Algeria katika Uwanja wa Taifa.

"Timu nyingi za kiarabu nazitambua hasa kutokana na uzoefu nilionao, nimefuatilia namna ambavyo wanafanya  na nimegundua kwamba wachezaji wao ni wajanja sana wanapiga sana kelele wakiwa uwanjani na wana mtindo wa kujiangushaangusha hilo lipo wazi nimeligundua na nimelifanyia kazi," alisema.

JS Saoura wametua jana Usiku wakiwa wameongozana na mtanzania Thomas Ulimwengu ambaye amesajiliwa msimu huu, huku wakiwa wamebeba maji yao pamoja na chakula chao.


Mpya zaidi Nzee zaidi