.

1/11/2019

Sikuhitaji umaarufu - BillnassMsanii wa Muziki Bongo, Billnass amekuwa hakuhitaji kuwa sana maarafu ila alikuwa anafanya muziki kwasababu ni kitu ambacho anakipenda.

BillNass amesema kuwa kufanya kitu anachokipenda yeye inampa furaha huku akifanya muziki Mashabiki wakiwa wanaongezeka.

"Kwa mimi sikuhitaji sana umaarufu, nilikuwa nafanya muziki kwasababu ni kitu ambacho nakipenda na ni talent ambayo nimebarikiwa. Kwahiyo kufanya kitu ninachokipenda mimi inanipa furaha nikifanya muziki mashabiki wanavyoongezeka hiyo ni feedback nzuri kwa kile kitu ambacho nakifanya na ninakipenda kutoka moyoni," amesema Billnass kwenye kipindi cha Dadaz cha EATV.

Billnass kwasasa anatamba na wimbo wake aliofanya na Whozu unaoitwa 'Kwa leo'.