Uchaguzi wa Yanga wagomewa na Wanachama


Wanachama wa Tawi la Yanga – Pluijm Ilala, wameonyesha hali ya kugomea uchaguzi wa klabu hiyo ambao wagombea wake wapo katika hatua ya kupiga kampeni za mwisho kuelekea kwenye hatua ya kupiga kura keshokutwa Jumapili katika Bwalo la Polisi Oysterbay.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Said Amanzi ameeleza kuwa wamelazimika kusambaza barua mbalimbali za maazimio ya wanachama wao wakiupinga uchaguzi huo kwa kile wanachodai hawawezi kushiriki jambo ambalo linakinzana na sheria na kanuni zilizopo kwenye katiba ya klabu hiyo.

 “Tunashangazwa sana na waziri mwenye dhamana ya hili kushindwa kuamua jambo dogo kama hili, kiasi kwamba kila kukicha wanakaa vikao ambavyo maamuzi yake yanakuwa ya upande mmoja na ya kusikitisha sana.

Pia amesema kama Waziri aligundua kuna makosa ya kimsingi iweje  hukumu ibaki kwa Yanga kusimamiwa uchaguzi wake wakati kamati yao ipo wazi na haihusiani na TFF na kwa nini TFF
wasingechukuliwa hatua.





Mpya zaidi Nzee zaidi