Wananchi wapandwa na gadhabu kutokana na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini

Wananchi wengi wamelalamika wakiishutumu shule moja katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Afrika Kusini kwa kuwatenganisha wanafunzi katika madarasa tofauti kulingana na rangi za ngozi zao.

Picha ambayo ilirushwa mitandaoni siku ya Jumatano imewaonyesha wanafunzi weusi wa chekechea wameketi katika kona ya darasa mbali na wanafunzi wenzao wazungu.

Picha hiyo imezua ghasia na ghadhabu miongoni mwa wananchi kwani Afrika Kusini imejariu kupambana na kuushinda ubaguzi wa rangi miaka 25 iliyopita.

"Tunataka kuukemea utawala wa rangi nyeupe ambao bado upo Afrika Kusini," Matakanye Matakanye, katibu mkuu wa Chama cha Taifa cha Mashirika ya Usimamizi wa Shule, alikiambia kituo cha habari cha Anadolu kwa njia ya simu.

Amesema shirika lake linakemea tukio hilo na linataka wito wa ushirikiano wa wanafunzi wote shuleni.

"Kuna watu wengi wenye rangi nyeupe na sio wabaguzi wa rangi na kuna shule nyingi nzuri pia nchini Afrika Kusini, lakini inaonekana wachache bado wanaendelea na ubaguzi wa rangi," alisema, akiongeza kuwa wahalifu wanapaswa kutambuliwa na kutengwa.

Wakati huo huo, Sello Lehare, waziri wa elimu amewaambia waandamanaji shuleni kuwa idara ya elimu inakemea na kupinga yale yaliyotokea darasani humo.

Alisema mwalimu, ambaye aliwatenganisha wanafunzi, amesimamishwa kazi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

Hata hivyo, mwenyekiti wa kamati inayoongoza shule katika shule hiyo ameviambia vyombo vya habari kuwa picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii sio kinachotendeka shuleni humo.

"Hii ni shule bora yenye muda mrefu na imekuwa ikiunganisha watu tofauti kwa miaka mingi na hakujawahi kutokea kwa tukio la ubaguzi wa rangi katika shule hii," mwenyekiti wa shule hiyo amewaambia waandishi wa habari wa eneo la Enca, lakini hakuwa na ufafanuzi wa kueleza kwa nini wanafunzi walikuwa wamejitenga katika kona ya darasa hilo.

Mwaka jana, Tume ya Haki za Binadamu Afrika Kusini ilisema katika ripoti kwamba mifumo ya ubaguzi wa rangi na usawa wa utaratibu wa kikabila imebaki nchini Afrika Kusini licha ya kuumaliza ubaguzi wa rangi miaka miwili iliyopita.