.

1/11/2019

Jambo moja kuhusu Weusi na Wapoloo


Kundi la Weusi limeeleza maana ya neno Wapoloo kwenye wimbo wao Mpya waliupa jina hilo.

G Nako amesema kuwa  Wapoloo imetokana na Tabia fulani wahuni ukienda maskani zao huwaga ni wakimya.

"Wapoloo imetokana na Tabia fulani wahuni ukienda maskani zao huwaga ni wakimya lakini usije ukawachukulia kimya hawanaga maneno mengi, Ukiona kwenye video kama wamesizi ukisema wahuni ni kama wanainuka," alisema G Nako.

Kundi la Weusi wametoa wimbo wa Wapoloo ambao unafanya vizuri kwasasa na ni wimbo wao wa kwanza kwa mwaka 2019.