Rais Muhammadu Buhari ameshinda kiti cha urais kwa muhula wa pili, baada ya kumbwaga mpinzani wake, Atiku Abubakar.
Rais Buhari amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya pili kwa kushinda asilimia 56 ya kura dhidi ya mpinzani wake, Atiku Abubakar aliyepata asilimia 41.
Hata hivyo idadi ya wapiga kura ilikuwa chini ya 35% ya waliojiandikisha, ikiwa ni idadi ndogo zaidi tangu taifa hilo liingie kwenye mfumo wa vyama vingi.
Chama cha Buhari (APC) kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.
