Wanne wakamatwa na Polisi kwa wizi wa hati za viwanja


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa hati za viwanja, kubadili ramani za mpango mji na kuuza viwanja kwa njia ya utapeli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema watu wamekuwa wakipelekea migogoro ya ardhi kwa wananchi kutokana na tabia hiyo.

"Wanasababisha migogoro mingi ya ardhi katika Jiji letu la Dodoma, wanashirikiana na watumishi ambao sio waaminifu na kupelekea kuingilia mifumo ya halmashauri ya ardhi," amesema.

Amesema kuwa watuhumiwa wote wanahojiwa kuhusiana na kugushi nyaraka za ardhi na wamepekuliwa na nyaraka wamekutwa nazo na muda wowote watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi uatakapokamilika.