RC kuunda tume ya kuchunguza WAMACU


Na Timothy Itembe Mara.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adamu Kigoma Malima ameahidi kuunda Tume ya kuchunguza mwenendo mzima wa utekelezaji wa shuguli za Chama cha wakulima wa Mara (WAMACU) ili wakulima wawe na imani na chama chao pindi majibu yatakapo toka.

Tume hiyo inatarajia kufanyakazi ndani ya miezi miwili na kutoa majibu kwenye mkutano mkuu wa Wakulima wa Mara Cooperative Union Limeted (WAMACU) unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 7 mwaka huu.

Malima aliamua kuunda Tume hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Vyama vya msingi vya ushirika wa Mazao mkoani Mara ambao walihudhuria kikao cha kupokea taarifa ya ukusanyaji na uuzwaji wa Kahawa ya msimu 2018/2019 kilichofanika jana katika  ukumbi wa Moroni Galdeni Hotel iliyopo Mjini hapa.

Malima alisema kuwa Serikali imelenga kufufua Ushirika wenye nguvu na wenye tija kwa hali hiyo kama mkuu wa mkoa Mara aliyeteuliwa na Raisi awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kumwakilisha kwa hali hiyo anatekeleza na kusimamia malengo ya serikali hiyo.

“Kama mnataka kuwa na WAMACU ya siku zote mimi sina matatizo lakini nataka muwe na WAMACU mpya yenye tija ambayo inaviongozi ambao ni wabunifu wenye lengo la kuongeza uzalishaji wa kahawa ili wakulima wakaondokane  umasikini na kama kuna changamoto inayowakumba viongopzi wa WAMACU nitaunda Tume ya kuchunguza hizo changamoto na itatoa majibu mwezi wa Saba mwaka huu kwenye mkutano kama huu ambao nitaenda kuugarimia mimi”alisema Malima.

Mwenyekiti wa Amcos Nkongore,James Makoromu alisema kuwa mkuu wa mkoa Mara tusaidie sisi wakulima tunaumia kwasababu malipo tunayolipwa ya  kahawa na WAMACU hayaeleweki kwani malipo ya awali tulikubaliana kulipwa shilingi Alfu moja ili kusubiri malipo baada ya mauzo ya kahawa mnadani pia malipo yetu yanacheleweshwa bila msingi.

Wilyamu Ezekiel wa Amcos Nyandurumo alisema kuwa katibu wa WAMACU,Lukas Massa nitatizo kwasababu bajeti anayowasomea ya mapato na matumizi ya ukusanyaji na uuzwaji haiendani mfano deni la Benk ya NMB la mwaka 2015/2016 shilingi million 195 na kuwa hapo nyuma Benk hiyo ilikuwa inadai shilingi nmilion 65 inakuwaje zifike shilingi milioni 195.